Matthew 6

1Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni. 2Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.

3Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia, 4ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.

5Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao. 6Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako. 7Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.

8Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake. 9Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako. 10Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.

11Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku. 12utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu. 13Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.’

14Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi. 15Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

16Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. 17Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako. 18Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.

19Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba. 20Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba. 21Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.

22Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru. 23Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani! 24Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.

25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? 26Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?

27Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake? 28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha. 29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.

30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, ‘Je tutakula nini?’ au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?”

32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. 33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako. Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.

34

Copyright information for SwaULB